WANAWAKE WAHIMIZWA KUSIMAMIA MALEZI

Baada ya kufanikiwa kiuchumi Wanawake Nchini wameaswa kuzingatia mila na desturi zinazojenga na sio kubomoa na kuharibu kizazi cha baadae

Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoani Geita kilopambwa na ujumbe mzito wa kuwataka Wanawake Nchini kuoanisha mafanikio ya kiuchumi na utunzaji wa mila na desturi bora.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amesisitiza kuwa juhudi za Serikali za kumuinua Mwanamke kiuchumi hazina lengo la kubomoa misingi ya Familia, bali ni kupunguza ukatili Majumbani.

DKT. MWINYI ASHIRIKI MAZISHI YA MAMA WA KAMANDA DAIMA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Viongozi mbalimbali wa Serikali katika Maziko ya Bibi Sichana Is-haka Daima Mama Mzazi wa Kamanda Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKU) Kanali Makame Abdalla Daima.

Marehemu Sichana Daima Amefariki Jana wakati akitibiwa katika Hospitali ya Mkoa Lumumba. Awali Dkt. Mwinyi alishiriki Sala ya Maiti katika Msikiti wa Bumbwini Misufini. 

ZAIDI YA WATANZANIA 200 WAREJEA KUTOKA DUBAI

Zaidi ya Watanzania 200 waliokuwa wamekwama katika Nchi za Falme za Kiarabu kwa Siku kadhaa kutokana na vita vinavyoendelea kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran wamerejeshwa Nchini kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL kupitia Uwanja wa Ndege wa Dubai hadi Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

 

Subscribe to
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.