Miundombinu ya kisasa ya matumizi ya Teknolojia ni msingi muhimu wa kuimarisha Ufanisi wa shughuli za Kitakwimu kwa njia ya usahihi na uwezo wa kuchambua data kwa haraka na kutoa Taarifa zenye ubora wa hali ya juu.
Akizungumza katika Uzinduzi wa Mradi wa kuwajengea uwezo Watakwiku katika mifumo wa Teknologia Naibu Waziri wa Fedha na mipango Mh Juma Makungu Juma amesema matumizi ya Teknologia katika mifumo ya Kitakwimu yatawawezesha watakwimu kutoa Takwimu bora jambo litakaloiwezesha Serikali kupanga sera na mipango endelevu kwa Maendeleo ya Taifa .
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Salum Kassim Ali amewataka Watendaji hao kuyafanyia kazi mafunzo waliyoyapata ili kuleta mabadiliko ya kiutendaji na kuongeza wigo wa utowaji wa Takwimu kisasa na kuachana na Mifumo ya kizamani.
Mradi huo wa kuwajengea uwezo Watakwimu katika mifumo wa Teknologia ni wa Miaka miwili na unatekelezwa na Ofisi ya mtakwimu Mkuu Serikali zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Korea ya Kusini