Watoto Wanane Wakaazi wa Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani Wamefariki Dunia baada ya Kudhaniwa Wamekula Samaki aina ya Kasa akiwa na sumu.
Wakizungumza kwa masikitiko makubwa baadhi ya Wahawanga wa Tukio hilo akiwemo Ndg.Miza Kombo Bakari ambaye alipoteza Watoto wake Wawili Mmoja wa Miaka Miwili na Nusu na mwengine wa Miezi Mitano amesema hakufahamu chanzo cha tukio hilo.
Sheha wa Shehia hiyo Ndg.Haji Ali Sshaali amesema anasikishwa na Tukio hilo ambalo limepoteza Maisha ya Watoto Wadogo.
Daktari Dhama Wilaya ya Mkoani Ndg.Haji Bakar Haji amesema Jumla ya Wagonjwa 86 wamefikishwa Hospitali ambapo katika hao Nane tayari walishaaga Dunia na Wengine wapo katika Hospitali ya Abdallah Mzee Mkoani wanaendelea na Matibabu.
stories
standard