HUZUNI :WATOTO NANE WAFARIKI BAADA YA KULA SAMAKI AINA YA KASA

KISIWA PANZA

    Watoto  Wanane  Wakaazi wa Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani Wamefariki Dunia baada ya Kudhaniwa Wamekula Samaki aina ya  Kasa akiwa na sumu.

      Wakizungumza kwa masikitiko  makubwa   baadhi ya Wahawanga  wa Tukio hilo akiwemo Ndg.Miza Kombo Bakari  ambaye alipoteza Watoto wake Wawili  Mmoja wa Miaka Miwili na Nusu na mwengine wa Miezi Mitano  amesema hakufahamu chanzo cha tukio hilo.

     Sheha wa Shehia hiyo Ndg.Haji Ali Sshaali amesema anasikishwa na  Tukio hilo ambalo limepoteza  Maisha ya Watoto Wadogo.

    Daktari Dhama Wilaya ya Mkoani Ndg.Haji Bakar Haji amesema Jumla ya Wagonjwa 86 wamefikishwa Hospitali ambapo katika hao Nane tayari walishaaga Dunia na Wengine wapo katika Hospitali ya Abdallah Mzee Mkoani wanaendelea na Matibabu.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.