Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mh Simai Mohamed Said, amesema Mkakati wa Serikali kusisitiza Utalii wa kimazingira imelenga kuhamasisha Watalii wa Daraja la juu kuingia Nchini kwa idadi Nchini.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa eneo la Ujenzi wa Hoteli ya Four Seasons katika Kijiji cha Pongwe Pwani, amesema kuna Watalii wenye uwezo mkubwa wanahitaji kukaa katika Hoteli zenye mazingira ya asili.
Amesema kwa vile wamiliki wa Mradi huo wana uzoefu wa kufanya kazi katika Mataifa mbali mbali wazingatie mahitaji hayo, ili kuona wanapokea Wageni wa kipekee ili kuingiza kiasi kikubwa cha fedha Nchini katika kipindi kifupi.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya kazi uchumi na uwekezaji Khatib Mwadini Khatib, amesema matarajio yao ni kuona uwepo wa mradi huo unanufaisha wazawa kwa kushika nafasi za mbali mbali za ajira.
Nae Mkurugenzi raslimali Watu mamlaka ya kukuza uwekezaji Vuai Yahya Lada amesema jumla ya miradi 95 ya uwekezaji imesajiliwa katika Mkoa wa kusini ambapo itasaidia katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi