JITIHADA ZA PAMOJA ZINAHITAJIKA KUKUZA SEKTA YA UTALII

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale na Wadau wa Sekta hiyo wanahitaji kuwa na ushirikiano wa karibu ili kuondosha vikwazo vinavyoikabili Sekta hiyo ikizingatiwa kuwa ni tegemeo kwa Uchumi wa Zanzibar unaochangia zaidi ya asilimia 30 ya pato lake.

Ukatika Kikao kilichohusisha Wizara ya Utalii na mambo ya kale, wakuu wa Mikoa, Wilaya na Masheha, Waziri wa Wizara hiyo mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amesema Sekta ya Utalii inakabiliwa na matatizo kadhaa ambayo kutatuliwa kwake kunahitaji nguvu za Wadau mbalimbali huku Serikali ikiwa inafanya mageuzi ikiwemo Sera ili kufikia malengo.

MKAKATI WA SERIKALI KUSISITIZA UTALII WA KIMAZINGIRA IMELENGA KUHAMASISHA WATALII WA DARAJA LA JUU KUINGIA NCHINI KWA IDADI

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mh Simai Mohamed Said, amesema Mkakati wa Serikali kusisitiza Utalii wa kimazingira imelenga kuhamasisha Watalii wa Daraja la juu kuingia Nchini kwa idadi Nchini.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa eneo la Ujenzi wa Hoteli ya Four Seasons katika Kijiji cha Pongwe Pwani, amesema kuna Watalii wenye uwezo mkubwa wanahitaji kukaa katika Hoteli zenye mazingira ya asili. 

Subscribe to WAZIRI WA UTALII NA MAMBO YA KALE
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.