JITIHADA ZA PAMOJA ZINAHITAJIKA KUKUZA SEKTA YA UTALII

MH. MUDRIK RAMADHAN SORAGA

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale na Wadau wa Sekta hiyo wanahitaji kuwa na ushirikiano wa karibu ili kuondosha vikwazo vinavyoikabili Sekta hiyo ikizingatiwa kuwa ni tegemeo kwa Uchumi wa Zanzibar unaochangia zaidi ya asilimia 30 ya pato lake.

Ukatika Kikao kilichohusisha Wizara ya Utalii na mambo ya kale, wakuu wa Mikoa, Wilaya na Masheha, Waziri wa Wizara hiyo mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amesema Sekta ya Utalii inakabiliwa na matatizo kadhaa ambayo kutatuliwa kwake kunahitaji nguvu za Wadau mbalimbali huku Serikali ikiwa inafanya mageuzi ikiwemo Sera ili kufikia malengo.

Wakichangia katika Kikao hicho Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri wamekiri kuwepo matatizo katika Sekta ya Utalii ikiwemo utoaji holela wa Vibali, kupotoshwa kwa Utamaduni mambo yanayoweza kushusha hadhi ya Sekta hiyo.

Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na mambo ya kale Dkt. Aboud Suleyman Jumbe amesema watafanyia kazi ushauri uliotolewa na Wadau hao kwa lengo la kuyatafutia ufumbuzi matatizo yaliyopo.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.