KUKAMILIKA KWA KIWANDA CHA MWANI PEMBA, KUTATOA FURSA KWA WANANCHI KUPATA MAENDELEO MAKUBWA YA KIUCHUMI.

RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema kukamilika kwa Kiwanda cha Mwani Pemba, kutatoa fursa kwa Wananchi kupata maendeleo makubwa ya Kiuchumi.

Dk.Mwinyi ameeleza hayo  Chamanangwe Wilaya ya Wete katika uwekaji wa Jiwe la msingi kiwanda cha kusarifu Mwani,ikiwa ni shamra shamra kutimia miaka60 ya Mapinduzi Zanzibar na kusema kuwa hiyo ni ishara kuwa kisiwa cha Pemba kimefunguka Kiuchumi.

Waziri wa Biashara na maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban amewasisitiza Wananchi kuendeleza kilimo cha Mwani kwa kasi zaidi ili malengo ya kuwepo Kiwanda hicho yafikiwe.

akitoa taarifa za ujenzi wa Kiwanda hicho Mkurugenzi Mkuu wa ZASCO, Dkt. Massoud Rashid Mohammed amesema Kiwanda kitakapo kamilika kitakuwa na uwezo wa kusarifu tani elfu thalathini za Mwani.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.