KAMATI BLW IMERIDHISHWA NA UJENZI MNADANI DARAJANI

KAMATI YA MAWASILIANO, ARDHI NA NISHATI

Kamati ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi iimeridhishwa na hatua iliyofikiwa ya matengenezo ya Miradi ya Majengo Makongwe inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Zanzibar katika maeneo ya Darajani.

Kamati hiyo ambayo imepokea Taarifa ya Miradi ya matengenezo wa Majengo hayo na kufanya ziara ya kuangalia hatua iliyofikwa, Makamo Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi  Mhe. Aza Januari Joseph amesema inatoa matumaini kwa hatua iliyofikiwa ili kutoa fursa ya kutumika kwa Majengo hayo ya Biashara.

Naibu Waziri wa Ardhi na maendeleo ya Makazi Mhe. Salha Mohammed Mwinjuma amesema pamoja na mambo mengine Wizara itahakikisha Majengo yake yanakua katika kiwango bora pamoja na kuleta mandhari nzuri ya Mji.

Mkurugenzi Mkuu Shirika la Nyumba Zanzibar Mwanaisha Ali Said amefahamisha kuwa Miradi yote ya Shirka inayotekelezwa inalengo la kuongezea mapato kwa Shirika na Serikali.

Mradi wa jengo la mnadani Darajani, umegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni Mojana linatarajiwa kukamilika Mwezi Disemba Mwaka huu.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.