KAMATI BLW IMERIDHISHWA NA UJENZI MNADANI DARAJANI
Kamati ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi iimeridhishwa na hatua iliyofikiwa ya matengenezo ya Miradi ya Majengo Makongwe inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Zanzibar katika maeneo ya Darajani.
Kamati hiyo ambayo imepokea Taarifa ya Miradi ya matengenezo wa Majengo hayo na kufanya ziara ya kuangalia hatua iliyofikwa, Makamo Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi Mhe. Aza Januari Joseph amesema inatoa matumaini kwa hatua iliyofikiwa ili kutoa fursa ya kutumika kwa Majengo hayo ya Biashara.