Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya Zanzibar, imefanikiwa kukamata Dawa za kulevya aina mbalimbali zinazokadiriwa kufikia Kilo Mia Moja na Ishirini na tano.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Kanal Burhani Zuberi Nassoro, amesema Dawa hizo zimekamatwa katika Operesheni iliyofanyika Mwezi January katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mjini Magharibi.
Akizitaja Dawa zilizokamatwa ni Heroin,Methamphetamine, Hashi na Bangi ambazo ni Kiwango kikubwa kuwahi kutokea katika Historia ya Zanzibar na kingefanikiwa kuingia Mtaankingesababisha Maafa makubwa.
Akizungumzia hali ya Dawa za kulevya Zanzibar Kanal Burhani,amesema Mwaka 2023, Mamlaka kwa kushirikiana na Vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama ilifanya Operesheni mbalimbali na kufanikiwa kukamata Dawa za Kulevya zenye uzito wa Tani 1 nukta 35.