ZFF KUANZISHA ‘ZANZIBAR BLUE SUPER CUP’ JULAI MWAKA HUU

Mkataba

Shirikisho la Mpira la Miguu Zanzibar (ZFF) limeandaa Mashindano ya Timu za Taifa kutoka Maeneo Mbali Mbali Duniani, yanayotarajiwa kuanza Julai, 2024.

 

Kauli Hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati Ya Fedha Na Mipango wa ZFF, Awadh Maulid Mwita Huko Ofisi za Shirikisho, Mbuyu Mnene.

Amesema mashindano hayo yatatambulika kwa jila la 'Zanzibar Blue Super Cup' ambayo yatashirikisha timu za taifa kutoka maeneo mbali mbali dunia ikiwemo Congo, Oman na kadhalika.

Amesema katika kukamilisha mashindano hayo, siku chache zijazo ZFF itazindua Jezi za Timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) na zitatumika katika mashindano mbali mbali ndani na njee ya nchi.

Mbali na mambo mengine ZFF imeaingia makubaliano ya ushirikiano na Kampuni ya Zanzibar Digital Limited (ZAN Digital) kwa ajili ya kuitangaza taasisi kupitia mifumo mbali mbali watakayoitumia.

Mkataba huo umeshughudiwa na Makamu wa Rais wa ZFF, Abdallah Yahya Shamhun, Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango, Awadh Maulid Mwita na Mkurugenzi wa ZAN Digital, Mohammed Saleh.

hot
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.