Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab
Amewataka Wazazi na Walezi Kisiwa Pemba kuendeleza mashirikano ya pamoja na Walimu katika kuwasimamia Watoto wao kusoma ili Taifa lipate Watalamu wa Fani mbali mbali.
Ametowa Wito huo huko Skuli ya Dkt Salamu Ahmed Ndugu Kitu Chake Chake katika Mahafali ya Wanafunzi wa Kidatu cha Nne.
Amesema kupata ufaulu mzuri katika Masomo kunahitaji Malezi ya pamoja kati ya Mzazi Walimu pamoja na kamati ya Skuli ili kuepuka na vishawishi mbali mbali ambavyo vitakwamisha jitihada zao za Masomo kutokana na maendeleo ya Sanyansi na Teknologia.
Afisa elimu Wilaya ya Chake Chake Burahani Khimis Juma amewataka Walimu kuendelea kuwasimamia Wanafunzi hao katika Masomo yao nae Mwalim mkuu wa Skuli hiyo Khamis Said Othman amesema mafanikio yaliyopatikana Skulini hapo ni mashirikano yapamoja kati ya Walim Wazazi na Uongozi wa Skuli licha ya changamoto mbali mbli zinazo ikabili skuli hiyo.
Na katika Risala iliyosomwa na Mwanafuzi Mulhati Omari Mohammed amesema licha ya mafanikio hayo lkn bado Skuli hiyo inakubwa changamoto mbali mbali ikiwemo Dahalia ,Gari kwa ajili ya kupelake Mgonjwa Hospitali wakati akitokea Mgonjwa.