WAHITIMU WA MAFUNZO NGAZI YA SAJENT WATAKIWA KUONGEZA KASI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UDHALILISHAJI

WAHITIMU JESHI LA POLISI

    Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Idrissa Kitwana Mustafa amewahimiza Wahitimu wa Mafunzo  Ngazi ya Sajent kuendelea kupambana na udhalilishaji ili kuheshimu Haki za Binadamu

   Akifunga Mafunzo ya Uongozi Mdogo Ngazi ya Sajenti yaliofanyika katika Ukumbi wa Polisi Ziwani na kukabidhi Vyeti kwa Wahitimu 277 amewataka kuendeleza juhudi zaidi katika kupambana na uhalifu ili kuendana na Mabadiliko ya Teknolojia.

   Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Moses Nekemiya Fundi amewataka  Wahitimu hao kuzingatia uadilifu katika kazi zao ambao ni msingi bora wa kuongeza ufanisi wa Kazi.

   Naibu Kamishna na Mkuu wa ufuatiliaji Tathmini wa Jeshi la Polisi DCP Alute Makita amesema ni vyema Wahitimu hao kuwasimamia Vijana waliochini yao kwa kuzingatia haki ,Weledi kwa huduma bora ili kupunguza malalamiko kwa Jeshi la Polisi .

   Nao Wahitimu wa Mafunzo hayo wameahidi kuyafanyia Kazi Elimu waliyoipata kwa haki na Weledi ili kutumikia Jamii.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.