WACHEZAJI NA WADAU WA SOKA WAOMBA KUEKEWA AMBULANCE VIWANJANI

AMBULANCE WACHEZAJI

Wachezaji ,Wadau na  Makocha wamesema kukosekana kwa Gari ya kubebea Wagonjwa Viwanjani kunahatarisha Maisha ya wanamichezo.

Wazingumzia umuhimu wa Gari hizo wadau hao wamesema wamekua wakilazimika kutumia Gari za kwaida ambazo hazina huduma zozote za kuokoa Maisha ya Wachezaji.

Aidha wamesema hali ya Usalama kwa Wachezaji inaonekana kutotiliwa uzito katika Viwanja vya Michezo mbali mbali na vyombo vinavyo pewa jukumu la kuendesha Ligi Nchini .

Aidha wameleza kua kumekuwa na matukio mengi kwa Wachezaji kuanguka wakati wakitmiza majukumu yao  na baadhi yao kuumia  ikiwemo katika muendelezo wa Ligi kuu Soka Zanzibar.

Ikimbukwe kuwa mechi kati ya  Ngome na uhamiaji na Malindi na JKU katika Ligi  kuu PBZ ilitokea matukio kama hayo hali iyoleta taharuki kwa mashabiki walihudhuria kuangalia Mechi hiyo.

Jambo hilo lisipo angaliwa mapema linaweza kuleta matatizo kwa Wachezaji  hivyo Wadau na Wapenzi wa Soka Nchini wameiyomba   Serikali  na wanaoanadaaa Ligi  kulitia uzito jambo hilo ili kuweka hali za Wachezaji katika Mazingira wezeshi.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.