Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amesema Ujenzi wa Skuli mpya kutaondoa mrundikano wa Wanafunzi katika Madarasa.
Katika shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwenye uwekaji jiwe la msingi Skuli ya Kidichi Wilaya ya Magharibi A, amesema Serikali inakusudia kuondosha uhaba wa Madarasa unaosababisha Wanafunzi kusoma kwa mikupuo miwili.
Akitoa maelezo ya Kitaalamu Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na mafunzo ya amali Dkt.Mwanakhamis Adam Ameir amesema ujenzi wa Skuli hiyo ya Ghorofa mbili utagharimu Shilingi bilioni nne nukta tano, umeanza Mei Mwaka2023 naunatarajiwa kukamilika mwaka huu ili kuwawezesha Wanafunzi kusoma katika mazingira bora.
Mkuu wa Wilaya ya Magharib a Suzan Peter Kunambi amesema Serikali ya Mkoa inaridhishwa na hatua ya miredi ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani humo.