SHIRIKA LA WORLD VISION TANZANIA LIMEKABIDHI MIRADI WILAYA YA KILOSA

KUKABIDHI MIRADI

   Halmashauri Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro imekabidhiwa Miradi ya Maendeleo iliyopo Tarafa ya Ulaya kutoka Shirika la World Vision Tanzania ikiwemo Miradi ya Visima vya Maji vinavyotumia Nishati ya jua, Vituo vya Afya na Mradi wa Skuli ya Msingi Madudumizi, itakayowanufaisha zaidi ya Wananchi Elfu Kumi wa Eneo hilo.

    Akizungumza na Wakazi wa Eneo hilo mara baada ya kutembelea Miradi hiyo kabla ya kukabidhiwa ili kujionea na kujiridhisha ubora wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa  Shaka Hamdu Shaka amesema hali hiyo imetoakana misingi mizuri i,liyowekwa na Serikali kwa Asasi zisizo za Kiserikali.

   Kutokana na utekelezaji wa Miradi hiyo Mratibu wa World Vision Tarafa ya Ulaya  Elisei Chilala na  Meneja Kanda ya Kati na Nyanda za Juu Kusini World Vision  Pudensiana Rwezaula wamesema Miradi hiyo imejikita katika Maeneo ya Elimu, Afya na Maji.

   Kwa upande wake Meneja Ruwasa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Sospeter Lutonja anaeleza hali ya upatikanaji wa maji Wilayani hapa huku baadhi ya wanufaika wakifurahishwa na ubora wa Miradi ambayo imekabidhiwa Wilayani hapo.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.