Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeamua kuimarisha Mazingira bora ya Elimu ya juu kwa Wananchi wake.
Akizindua mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi Nchini Tanzania katika Taasisi ya Sayansi ya bahari huko Chukwani Naibu Mratibu wa Mradi huo Dkt liberato Haule amesema lengo la Mradi huo ni juhudi za Serikali za kuhakikisha wanaongeza mchango wa Elimu ya juu kwa maendeleo ya Uchumi wa Taifa.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi za bahari Dr Daud Msaugameno amesema Mradi huo utakuwa na manufaa ya uimarishaji wa Miundombinu mbali mbali ya kufanyia kazi.
Diwani wa Wadi ya Chukwani Fatma Rashid Juma amewapongeza Watu wa Taasisi wa Mradi huo na kuahidi watashirikiana nao ili kutumiza lengo la Serikali.
Mtaalumu wa mambo ya mazingira Chuo Kikuu cha Dar Es Saalam Dr Edimund Mabwiye amesema wanatarajia Miundo mbinu iliyowekwa itaweza kuongeza Tija na maarifa pamoja na maendeleo endelevu Nchini Tanzania.