Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Amewahamasisha Viongozi Kuwasaidia Wananchi Hasa Katika Kipindi Cha Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani Ili Kuweza Kuweka Uwiano Sawa Wa Mahitaji.
Mhe. Hemed Ambae Ni Mwakilishi Wa Jimbo La Kiwani, Ametoa Wito Huo Baada Ya Ugawaji Wa Futari Kwa Wananchi Wa Jimbo Hilo Shehia Ya Kendwa Yenye Nyumba Zaidi Ya 1156 Hafla Iliyofanyika Kwenye Uwanja Wa Mpira Wa Mauwanifutari Kwa Wananchi Wote Hasa Wenye Mahitaji Maalum.

Kwa Upande Wake Mfanya Biashara Said Nassir Nasor (Bobar) Ameishukuru Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Kwa Kuendelea Kumpatia Ushirikiano Ambapo Kwa Mwezi Huu Wa Ramadhani Amepatiwa Usafiri Wa Kusafirisha Bidhaa Mbali Mbali Ambazo Atawakabidhi Wananchi Wa Kisiwani Pemba.

Nao Wananchi Waliopatiwa Sadaka Hizo Wamemshukuru Mwakilishi Wao Kwa Kuendelea Kuwatumikia Kwa Moyo Wa Upendo, Huruma Na Usawa Kwa Wananchi Wote Jimboni Humo Jambo Ambalo Linawapa Faraja Na Imani Kubwa Juu Yake.
