MASHEHA NA MADIWANI KUYASIMAMIA VYEMA MAENEO YAO

MHE MASOUD ALI MOHAMMED

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na idara maalum za SMZ  ,Mhe Masoud Ali Mohamed, amewasisitiza Masheha na Madiwani kuyasimamia vyema maeneo yao, ili kuimarisha ulinzi na usalama katika shehia zao.

Akizungumza na masheha, madiwani na Watendaji wa Wilaya ya Kusini huko Makunduchi, amesema kuwepo kwa Mikakati imara watakayoyaanzisha kutasaidia pia kuvidhibiti Vikundi vya uhalifu na Wananchi pamoja na Wageni wataendelea kuishi katika hali ya usalama.

Aidha Mh Masoud amewataka Watendaji hao kudhibiti ujenzi Holela unaendelea katika maeneo yasio rasmi ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza huku akisisitiza kuimarisha usafi katika Wilaya hiyo ambayo imekuwa ni ukanda Kitalii. 

Mkuu wa Wilaya ya Kusini  Galos  Nyimbo, amewataka Watendaji wa Ofisi hiyo kuhakikisha wanatekeleza Majukumu yao kwa ufanisi ili kufikia malengo yaliyokusudia.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.