BARABARA YENYE UREFU WA KILOMITA 2.4 KUFUNGULIWA
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe. Masoud Ali Mohamed ameipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa juhudi inazozichukua katika kuimarisha ujenzi wa miundombinu ya barabara.
Mhe. Masoud ameeleza hayo wakati akiizindua rasmi barabara ya Mgeni Haji-Kwambani yenye urefu wa kilomita 2.4.
Amesema juhudi zinazochukuliwa na Serikali wananchi wanapaswa kuzilinda na kuzitunza barabara ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.