Klabu ya Simba SC, imetangaza rasmi kuisadia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutangaza Utalii wa visiwa hivi, kwa kutembelea maeneo yenye vivutio vya Utalii pamoja na kuvaa Jezi zilizoandikwa 'Visit Zanzibar' katika michezo yao ya Michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Simba itaanza kuvaa Jezi zilizoandikwa 'Visit Zanzibar' kwenye Mchezo wao wa Pili dhidi ya Singida Fountain Gate unaotarajiwa kuchezwa kesho majira ya saa mbili na Robo usiku katika Uwanja wa New Amaan Complex.
"Sisi kama Klabu ya Simba tunawajibu wa kusaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutangaza Utaliii kupitia michezo hivyo tutatembelea maeneo ya kihistoria na kuvaa Jezi zilizoandikwa 'Visit Zanzibar'
“Tunazungumzia uchumi wa Zanzibar na uchumi wa Tanzania. Simba mwaka huu tumekuja kushiriki Mapinduzi Cup lakini pia tutakuwa na shughuli nyingi nje ya mashindano ambayo itakuwa ni kusaidia kutangaza utalii wa Zanzibar kwa kutumia mitandao yetu.”
“Hii sio mara ya kwanza Simba kutangaza utalii, wote mnakumbuka kwenye CAF tulikuwa tunatangaza Visit Tanzania na sasa tunatangaza utalii wa Zanzibar kwa kuanzia kesho.”
“Kama Simba kupitia mitandao yetu ya kijamii watu wengi Afrika na duniani watakuja kutembelea Zanzibar. Lengo letu ni kuisaidia Zanzibar katika eneo hilo na tayari kuanzia jana tulianza kutumia
“Sisi ni maendeleo, Zanzibar inapiga hatua kubwa sana, na sisi kama klabu kubwa tumeona ni vyema kuunga mkono juhudi za serikali. Jambo hili litasaidia kukuza uchumi na watu watapata fedha ambazo watakuwa wanatumia kama mambo ya maendeleo, kununua jezi, kununua bidhaa mbalimbali za klabu na hata kuja kwenye mechi. Tutatumia siku ambazo hatuchezi mechi kutangaza maeneo ya kitalii.”- alisema Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Iman Kajula.
Mchezo wa kwanza kwa Simba katika michuano hiyo, alifanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 3-1 dhidi ya JKU, usiku wa jana.