Timu ya Simba SC imefanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kuifunga Singida Penaty 3-2 huku dakika 90' za mchezo huo zikikamilika kwa sare ya bao 1-1 katika viwanja vya New Amaan Complex, Zanzibar
Singida ndio waliyotangulia kupata bao kupitia mchezaji Elvis Rupia dakika ya 16 ya mchezo huku bao la kusawazisha la Simba likifungwa na kiungo, Fabrice Ngome dakika ya 97' ya mchezo huo.
Simba ataungana na Mlandege katika fainali ya michuano ya Mapinduzi, Jumamosi, Januari 13, 2024, saa 2:15 usiku, Viwanja vya New Amaan Complex, mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
hot
standard