Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria utumishi na utawala bora, Mh Haroun ali suleiman, amesema Serikali itaendelea kuvitumia vikosi vya idara maalum za SMZ katika ujenzi wa Miradi ya Maendeleo.
Akifungua Soko la Matunda na Mbogamboga Donge Mtambile, Waziri Haroun amesema Miradi ya Ujenzi iliyosimamiwa na Vikosi hivyo imeonekana kuwa ya kiwango na kuwataka Wananchi kulitunza Soko hilo kwani ni chanzo muhimu cha kuwainua kiuchumi na kuongeza Pato la Serikali.
Akitoa taarifa kuhusu Ujenzi huo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ, Issa Mahfouh Haji, amesema soko hilo litawanufaisha wananchi kwa kuinua hali zao za kimaisha na kuwawezesha vijana kujiajiri.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Rashid Hadid Rashid amewaomba Wananchi kulitumia Soko hilo na kuacha kutumia maeneo yasiyo Rasmi kwa usalama wao na wanaofata huduma.
Ujenzi wa Soko hilo umejengwa na Kikosi cha Valantia KVZ umezingatia Wananchi wa hali zote.