Vigogo wa La Liga, Real Madrid walipata ushindi mnono dhidi ya Mallorca kutokana na bao la kichwa la Antonio Rudiger.
Mallorca iligonga mbao mara mbili huku mpira wa kichwa wa Antonio Sanchez ukipita chini ya mwamba wa goli hadi langoni, huku Samu Costa pia akigonga nguzo kwa wageni.
Makosa hayo yalikuwa ya gharama kwani Rudiger alifunga kwa kichwa akiunganisha kona nzuri ya winga ya kushoto ya Luka Modric dakika ya 78.
Real sasa hawajafungwa katika michezo 18 katika mashindano yote wanayocheza.
Matokeo hayo yameifanya Real ifikishe alama tatu kileleni kwa muda mfupi, kabla ya Girona iliyo nafasi ya pili kurejea kwa alama kutokana na bao la ushindi la dakika ya 91 kutoka kwa Ivan Martin walipoilaza Atletico Madrid walio nafasi ya tatu kwa mabao 4-3.
Real na Girona wana pointi 48 baada ya mechi 19 katika nusu ya msimu wa ligi ya Uhispania, huku timu hiyo ya Madrid ikiwa kileleni kutokana na tofauti nzuri ya mabao.