NYOTA WA BARCELONA, KUKAA NJEE BAADA YA KUPATA MAJERAHA

Barcelona

Beki wa Barcelona, ​​Inigo Martinez anakabiliwa na kipindi kingine cha kukaa nje ya uwanja baada ya kupata majeraha mapya aliporejea uwanjani wikendi.

 

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania alidumu kwa dakika 11 pekee aliporejea kutoka kwa tatizo la msuli wa paja kama mchezaji wa akiba katika kipindi cha pili katika ushindi wa Copa del Rey Jumapili huko Barbastro.

 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 sasa ana jeraha la paja na, akiwa amekaa nje kwa mwezi mmoja, sasa anakabiliwa na kipindi kingine kwenye orodha ya majeruhi.

 

Taarifa kutoka klabu hiyo inasema Majaribio yaliyofanywa kwa mchezaji wa kikosi cha kwanza yanaonyesha kwamba Inigo Martinez ana jeraha la misuli ya biceps femoris kwenye paja lake la kushoto na anatarajiwa kurudi uwanjani muda sio mrefu baada ya matibabu.

hot
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.