Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Hussein Ali Mwinyi ameuagiza mfuko wa hifadhi ya jamii ZSSF kuendelea kutafuta Kampuni za uhakika za uwekezaji hasa Mabasi ya kisasa yanayotumia Umeme au Gesi asilia ili kuwarahisishia Wananchi huduma ya usafiri.
Ametoa agizo hilo baada ya uwekaji wa Jiwe la msingi kituo cha Mabasi cha kisasa Kijangwani ikiwa ni shamra shamra za kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar amesemautaratibu huo utaondoa vurugu katika Nchi kwani kutakuwa na usafiri wa uhakika ambapo pia itaiweka Nchi kuwa na mabadiliko makubwa ya usafiri.
Aidha Dkt Mwinyi amefahamisha kuwa Zanzibar ni sehemu ya Dunia hivyo ni hatua nzuri kwa Nchi kuwa na eneo hilo la makutano ya usafiri ambao utatoa haiba ya Mji na kuwa na usafiri wa uhakika huku akiutaka mfuko wa ZSSF kufikiria kujenga kituo kidogo maeneneo ya Mnazi Mmoja ili kuongeza pato la Taifa.
Waziri wa Nchi afisi ya Rais Fedha na Mipango Dkt Sada Mkuya Salum amesema uwekezaji huo unaofanywa na ZSSF ni hatua nzuri katika kuleta maendeleo ya Nchi.
Mkurugenzi mwendeshaji wa ZSSF Nassor Shaaban Ameir amesema Ujenzi wa Kituo hicho umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 8 ambao Miradi huo unalengo la kuwasaidia wananchi huduma za usafiri.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Idrisa Kitwana Mustafa amepongeza hatua ya Rais kwa kuendeleza Miradi ya maendeleo na kuahidi kuunga mkono.