JAMII YA MASASI MKOANI MTWARA WADUMISHA MILA NA DESTURI ZA UNYAGO

Jamii ya Masasi

    Wakazi wa jamii ya Masasi Mkoani Mtwara wadumisha Mila na desturi za unyago wa kimila

     Wakazi wa kijji cha Nangoo wamekiri kudumisha Mila zao Kila ifikapo mwezi wa 6 na mwezi wa 12 na kwa watoto waliofikia umri wa miaka 7 mpaka 10 wakike na kiume upelekwa porini kupata mafunzo ya kimila yenye lengo la kuwafanya watoto kua na heshima,  kujituma, nidhamu pia kufanya vizuri katika kazi mbali mbali.

     Ndugu Venant Isaya Gabriel Mwenyekiti wa kijji cha Nangoo amekiri kutokea kwa mila hizo maarufu unyago katika miezi hio

     Kwa upande wa Kiongozi wa Kijadi yaani ngariba wa kijjini hapo maarufu kama Kokoliko nae amesema hio ndiyo kazi yake ya kutairi watoto, kuzindika na kutoa mafunzo kwa watoto wakiwa porini. kokoliko amesema watoto hukaa porini muda wa mwezi mmoja wakipewa mafunzo.

    Kwa upande wa Wananchi wa Nangoo wanaomba jamii isidharau mila na desturi kwani ni muhimu sana kwa ajili ya malezi ya watoto na ni kitambulisho cha Taifa, unyago ni miongoni mwa Mila na desturi kwa makabila ya Wamakua, Wayao, Wamwera, Wamakonde, Wangoni yani makabila ya Kusini.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.