TAASISI YA MWANAMKE INITIATIVES INA MCHANGO MKUBWA KUSAIDIA SERIKALI

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe Lela Mohamed Mussa, amesema, Taaisisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF)  ina mchango katika kusaidia Serikali na kusaidia upatikanaji wa matokeo  katika Mitihani  ya Taifa Zanzibar.

Amesema katika Uongozi wao wamekuwa Mstari wa mbele kusaidia ikiwemo kutatua matatizo  yanayowakabili Wanafunzi na kuwaandalia Kambi maalum ya masomo jambo ambalo limesababisha kupatikana Matokeo mazuri katika Mitihani yao ya Taifa.

Waziri Lela ameyasema hayo katika uzinduzi wa Upishi Salama Project katika Kiwanja vya Skuli ya Hasnuu Makame Mkoa wa Kusini Unguja amesema, Taasisi hiyo ina lengo la kuendeleza Elimu na kumuwezesha Mwanamke katika nafasi mbalimbali.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation(MIF) Mh  Wanu Hafidh Ameir, amesema, Taasisi hiyo inachukua jitihada mbalimbali ikiwemo kuweka mazingira bora ya upatikanaji wa Elimu na kuondosha usumbufu mdogo mdogo katika kupata elimu na kupika  kwenye mfumo wa matumizi ya Gesi ili kuondokana na Madhara ya utumiaji wa Kuni ili kuhifadhi Mazingira.

Meneja wa Benki ya Equit Sekta ya Umma na Utawala wa Tasisi Johanes Msuya  amesema Benki hiyo ni Mdau wa mambo ya Elimu kwani ni muhimu kutunzwa mazingira na kuepukanana na  athari za mabadiliko ya Tabia ya Nchi na wataendelea kusaidia Serikali katika nyanja  mbali mbali.

Akitoa shukrani kwa Niaba ya uongozi wa Skuli ya Hasnuu Makame, Msaidizi Mkuu Skuli ya Hasnuu Makame, Issa ali Haji, na Mkuu wa Jiko Haji Khamis Juma wamesema Taasisi hiyo inashirikiana na katika kutatua matatizo yalipo katika Skuli hiyo.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.