UWEKEZAJI UNAHITAJI KUWEPO KWA MIFUMO IMARA YA UTOAJI HAKI

RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema uwekezaji wa Miradi ya Kiuchumi unahitaji uwepo Mifumo imara wa utoaji haki.

Akizungumza kwenye Maadhimisho ya 13 ya Siku ya Sharia, kwenye Viwanja vya Mahakama Kuu Tunguu, Dkt Mwinyi amesema Zanzibar inashuhudia ongezeko la wawekezaji kwenye miradi mbalimbali zikiwemo ujenzi wa Hoteli, Viwanda na miradi mingine, jambo ambalo linahitaji uwepo wa mifumo imara ya upatikanaji haki uwazi, na kwa wakati.                                                    

Aidha Dkt Mwinyi amesema ustawi wa Wananchi kwa kiasi kikubwa utategemea uwepo wa misingi imara ya kuheshimu haki za Binaadamu, utawala bora, uhuru wa Mahkama na sheria zinazoilinda Jamii dhidi ya aina zote za unyanyasaji.                                   

Mapema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala bora Haroun Ali Suleiman, amesema Jitihada kubwa zilizochukuliwa na Serikali  za kujengewa mahakama za kisasa wanatarajia kuwa usikilizwaji wa kesi utakuwa wa kasi zaidi.      

Naye Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla amesema Jukumu la Msingi la Mahakama ni kupokea, kusikiliza na kuyatolea maamuzi mashauri ya Jinai na Madai, hivyo amewataka Wananchi, Taasisi za Serikali na Binafsi kuwaripoti kwenye Kamati ya Maadili, Watumishi wote wa Mahakama ama Mawakili wa kujitegemea ambao watakiuka maadili ya kazi zao ili wachukuliwe hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria.

Katika Hafla hiyo Dkt Mwinyi amezindua Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahkama (2024-2029) na kukabidhiwa Ripoti ya Utendaji kazi wa Mahkama ya Mwaka 2023. 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.