DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AMEELEZEA KURIDHISHWA NA VIWANGO VYA UJENZI WA BARABARA YA UWANJA WA NDEGE-MNAZIMMOJA

RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi dkt. Hussein Ali Mwinyi ameelezea kuridhishwa na viwango vya ujenzi wa Barabara ya Uwanja wa Ndege-Mnazimmoja amesema kuwa itakuwa ya mfano na inaendana na kasi ya ukuaji uchumi wa Zanzibar.

Dkt. Mwinyi akizungumza katika uwekaji Jiwe la Msingi wa Ujenzi wa Bara Bara hiyo   yenye urefu wa Kilomita 6 nukta 8, amesema Serikali lengo la Serikali ni kuona Barabara zote zinajengwa kwa kiwango bora ili zitumike kwa muda mrefu huku akiwataka Wanachi kuacha kufanya Biashara pembezoni mwa Barabara.

Waziri wa ujenzi mawasiliano na uchukuzi Dkt. Khalid Salum Mohd amesema Serikali ina malengo makubwa zaidi ya kuimarisha usafiri wa aina zote ili kurahisisha shughuli za Wananchi pamoja na Serikali.

Mbunge wa Jimbo  la Kikwajuni Mhandisi Hamad Yusuf  Masauni amesema   Wananchi wa jimbo hilo wameanza kufaidika na Ujenzi wa Bara Bara   za ndani huku akisifu maendeleo yaliyofikiwa.

Barabara hiyo inajengwa na Kampuni ya ujenzi ya CCECC ya China kwa kuzingatia viwango vya Kimataifa.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.