Michuano ya Kombe la Mapinduzi, hatua ya robo fainali inatarajiwa kuanza kesho, Januari 7, 2024 katika viwanja vya Amaan Sports Complex.
Timu nne zinatarajiwa kushuka dimbani, wakiwemo Mabingwa watetezi wa michuano hiyo, klabu ya Mlandege wakiwakaribisha kikosi cha Valantia Zanzibar, timu ya KVZ saa kumi na robo jioni na mchezo wa robo fainali ya pili ni saa mbili na robo usiku itakuwa ni kati ya Yanga dhidi ya APR ya Rwanda.
Hatua hiyo ya robo kuendelea tena Januari 8, 2024 mchezo wa mapema itakuwa kati ya Mabingwa wa kihistoria wa kombe hilo klabu ya Azam FC dhidi ya Singida huku mchezo mwengine majira ya saa mbili na robo usiku itakuwa kati ya Simba dhidi ya Jamhuri.
Timu zilizoaga mashindano katika hatua ya makundi ni Vital'o ya Burundi, Chipukizi, Jamus ya Sudani Kusini na JKU.