Mamlaka zinazosimamia Usalama wa Barabarani pamoja na Waendesha Pikipiki (bodaboda) wametakiwa kuchukuwa hatua za Kisheria pamoja na kusimamia vyema Ajali zinazojitokeza kila siku.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dkt. Khalid Salum Mohamed ameeleza hayo wakati akizungumza na Vyombo vya usalama pamoja na Wawakilishi wa waendesha BodaBoda na kusema kuwa kutokana na ongezeko la Ajali, ni vyema kuzingatia matumizi ya Barabara pamoja na kutii Sheria.
Mwanasheria wa Mamlaka ya usafiri na Usalama Barabarani Hassan Vuai amebainisha sababu zinazochangia Ajali ni pamoja na Madereva wengi kutokuwa na Leseni pamoja na kukosa Mafunzo ya huduma za Usafirishaji.
Kamanda wa Zoni ya Kusini Unguja Sacap, Daniel Shillah amesema Elimu inahitajika kutolewa kwa Jamii kwa lengo la kutambua Wajibu wao kufanya hivyo itaweza kupunguza Ajali zinazojitokeza.
Ajali 96 zimeripotiwa hususan usafiri wa Pikipiki kwa Mwaka 2023.