KARUME BOYS U-15 YAKABIDHIWA MILIONI MIA MOJA NA SITA, LAKI SABA NA TISINI.

Picha

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar imekabidhi kiasi cha fedha kwa timu ya taifa ya Zanzibar kufuatia harambee iliyofanywa katika fainali waliyoifunga Uganda na kutwaa Ubingwa wa CECAFA chini ya umri wa miaka 15 hivi karibuni.

Katika harambee hiyo kiasi kilichopatikana ni Shilingi Milioni Mia Moja na sita, laki Saba na Tisini huku kila mchezaji amekabidhiwa Shilingi Milioni Mbili na Laki Tisa kwa wachezaji 25 na Viongozi 10, ambapo Jumla ni 35 wanaounda Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15.

Akizungumzia kuhusu kuchelewa kwa zoezi hilo, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fatma Hamad amesema baadhi ya watu na Kampuni mbali mbali walichelewa kukabidhi fedha walizoahidi, ambapo hadi hivi sasa wapo ambao hawajatimiza ahadi waliyoiweka, jambo ambalo limepelekea kukamilika kwa wakati wa zoezi hilo. 

Karume Boys ilitwaa Ubingwa wa CECAFA miezi miwili iliyopita baada ya kuwafunga wenyeji Uganda penaty 4-3 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 90' za fainali hiyo.

hot
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.