Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno-Hatta, Tangerang Mjini Jarkata Nchini kwa ajili ya ziara ya Kitaifa Nchini Indonesia inayoanza 24 Januari, 2024.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno -hatta, Tangerang Raisi Samia alipokelewa na Naibu Waziri wa mambo ya Nje wa Indonesia Vice Pahala Nugraha Mansury.
Ziara hio ya siku tatu imekuja kufuatia mualiko wa Raisi wa Indonesia Mh. Joko Widodo ambae alifanya ziara Nchini Tanzania Agosti 2023.
stories
standard