Bondia Mtanzania, Hassan Mwakinyo anatarajiwa kushuka ulingoni tena Januari 27, 2024 kwenye ukumbi mpya wa ndani ya New Amaan Complex visiwani Zanzibar kupambana na Bondia wa Zimbabwe, Enock Msambuzi kwenye pambano litakalofahamika kama pambano la #MtataMtatuzi
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Bondia huyo amesema amejiandaa vyema kuja kuonesha burudani na mpambano mkali ambao utakuwa ni zawadi kwa mengi mazuri yaliyofanywa na Rais wa Zanzibar kwenye kuboresha miundo mbinu ya michezo Zanzibar.
Pambano hili lililoandaliwa na Peak Time Promotion kwa kushirikiana na ZBC, PBZ BANK ZRA na ZIPA litakuwa na mapambano mengine kadhaa ya utangulizi ya mabondia wa ndani na nje ya Zanzibar ambapo pia itakuwa ndio uzinduzi rasmi wa ukumbi huo mpya uliopo ndani ya viwanja vya Amaan Complex Zanzibar utakaokuwa ukitumika kwenye shughuli mbalimbali za michezo na burudani.
Hivi karibuni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi aliufungua rasmi Uwanja huo huo na kuupa jina la New Amaan Complex, Disemba 27, 2023.
Ni muda mrefu umepita Bondia Hassan Mwakinyo hajaonekana Ulingoni, hivyo Pambano hilo linatadhamiwa kuwa ni la aina yake, Zanzibar, Tanzania na Duaniani kwa ujumla.