WIZARA YA NISHATI IMEKABIDHI VITENDEA KAZI KWA TANESCO KUIMARISHA HUDUMA

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba akikabidhi vitendea kazi kwa Shirika la umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Shinyanga
English

Wizara ya Nishati imechukuwa  hatua mpya ya kuimarisha huduma za umeme Mkoani Shinyanga  baada ya Shirika la Umeme Tanzania  TANESCO kupatiwa vitendea kazi vitakavyorahisisha kuwafikia wananchi wengi zaidi, hususan waishio vijijini na maeneo ya pembezoni.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vitendea kazi , Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema uwekezaji huo ni sehemu ya jitihada za kuhakikisha umeme unawafikia wananchi wote bila kujali mahali walipo.

Vifaa vilivyo kabidhiwa ni pamoja na magari manne, bajaji moja na pikipiki mbili, vifaa ambavyo  vitaongeza  kasi ya utoaji huduma na ufanisi wa shirika hilo.

Amewahimiza wananchi kuanza kutumia majiko ya umeme kama njia ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi, akibainisha kuwa hatua hiyo itasaidia kulinda mazingira na kupunguza athari za kiafya zitokanazo na matumizi ya kuni na mkaa.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Benson Mbigili, amesema vitendea kazi hivyo vitaongeza uwezo wa kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuboresha huduma kwa kiwango kikubwa na kuchochea kasi ya utekelezaji wa miradi ya umeme na kusaidia kufikia malengo ya taifa.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.