WIZARA YA NISHATI IMEKABIDHI VITENDEA KAZI KWA TANESCO KUIMARISHA HUDUMA
Wizara ya Nishati imechukuwa hatua mpya ya kuimarisha huduma za umeme Mkoani Shinyanga baada ya Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kupatiwa vitendea kazi vitakavyorahisisha kuwafikia wananchi wengi zaidi, hususan waishio vijijini na maeneo ya pembezoni.

