Waziri wa Nchi Afisi ya Rais katiba Sheria, Utumishi na Utawala bora Mhe. Haroun Ali Suleiman amesema ni jukumu la wakuu wa Taasisi na vitengo kukaa pamoja kujadili namna ya kuwaelimisha Watendaji wao juu ya utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma.
Akifungua Mkutano wa Kamisheni ya Utumishi wa umma Zanzibar na Taasisi zinazojitegemea na Wakala Tendaji wa SMZ, Mhe Haroun amesema serikali imeweka sheria na kanuni bora za Utumishi lakini tatizo ni kushindwa kuzitafsiri na kuzitekeleza ambapo Wafanyakazi wengi hufanyakazi kwa mazowea bila kuzielewa Sheria hizo.
Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma kubingwa Mashaka Simba amesema Kamisheni hiyo imeshafanya Mkutano kama huo kwa lengo la kusimamia na kuimarisha Utawala bora na Sekta ya Utumishi wa Umma.
Wakiwasilisha mada katika Mkutano huo Wakurugenzi Kamisheni ya Utumishi wa umma wamesema baadhi ya kasoro zilizobainika katika Taasisi za Umma ni kuwa Taarifa za Watumishi kutohifadhiwa katika Mfumo wa Kielektronic.
Nao washiriki ameomba Taarifa za ukaguzi wa Watumishi wa Umma ziwekwe wazi ili kuimarisha uwajibikaji kwa Watumishi hao kwa Taasisi zao.