VIONGOZI NA WAKUU WA TAASISI WAMESISITIZWA KUSIMAMIA UWAJIBIKAJI.

WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS KATIBA SHERIA UTUMISHI NA UTAWALA

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais katiba Sheria, Utumishi na Utawala bora Mhe. Haroun Ali Suleiman amesema ni jukumu la wakuu wa Taasisi na vitengo kukaa pamoja kujadili namna ya kuwaelimisha Watendaji wao juu ya utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma.

Akifungua  Mkutano wa Kamisheni ya Utumishi wa umma Zanzibar  na Taasisi zinazojitegemea  na Wakala Tendaji wa SMZ, Mhe Haroun amesema  serikali imeweka sheria na kanuni bora za Utumishi lakini tatizo ni kushindwa kuzitafsiri na kuzitekeleza  ambapo Wafanyakazi wengi hufanyakazi kwa mazowea  bila kuzielewa Sheria hizo.

Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma kubingwa Mashaka Simba amesema Kamisheni hiyo  imeshafanya Mkutano kama huo kwa lengo  la kusimamia na  kuimarisha Utawala bora na Sekta ya Utumishi wa Umma. 

Wakiwasilisha mada katika Mkutano huo Wakurugenzi Kamisheni ya Utumishi wa umma   wamesema baadhi ya kasoro zilizobainika katika Taasisi za Umma  ni kuwa Taarifa za Watumishi kutohifadhiwa katika Mfumo wa Kielektronic.

Nao washiriki ameomba Taarifa za ukaguzi wa Watumishi wa Umma ziwekwe wazi ili kuimarisha uwajibikaji kwa Watumishi hao kwa Taasisi zao.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.