VIFO VYA MAMA NA MTOTO VYAFIKIA 20 KWA MWEZI JANUARI HADI MACHI

MHE. NASSOR AHMED MAZURUI

Waziri wa afya Mhe Nassor Ahmed Mazrui amesema kwa kipindi cha Januari hadi Machi Vifo vya Mama na Mtoto vilivyoripotiwa ni 20 kutokana na sababu mbali mbali zikiwemo upungufu wa watoa huduma pamoja na ukosefu wa Vifaa Tiba bora katika Hospitali. 

Akizungumza katika makabidhisho ya Vifaa Tiba kupitia Programu ya Uzazi ni Maisha Wogging Mhe Mazrui amesema Serikali itaendelea na kuchukua juhudi mbali mbali ili kupunguza vifo hivyo.

Meneja Mradi kutoka AMREF Dkt Sarafina Nkuwa amefahamisha kuwa mpaka sasa wamevisaidia Vituo 28 vinavyotoa huduma ya Mama na Mtoto Nchini hivyo ameahidi kuendelea kuisaidia Sekta ya Afya kupitia Vifaa TIba mbali mbali ili kutoa huduma bora ya Mama na Mtoto hasa wakati wa kujifungua.

Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt Salum Slim amesema Shilingi Milioni Mia Tisa imelenga kuwasaidia hudumza ya Mama na Mtoto huko ametoa Shukrani kwa Msaada huo ambapo Meneja wa Biashara Benki ya NMB Naima Said Shaame amesema miongoni mwa vipaumbele vya Benki hiyo ni afya ili kuona Mama na Mtoto anakuwa salama.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.