MAJESTIC CINEMA KUFANYIWA MATENGENEZO

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Kimataifa (UNESCO) linatarajia kulifanyia matengenezo Jengo la Majestic Cinema la Mji Mkongwe na kuwa Kituo Kikuu cha Utamaduni.

Akizungumza katika Warsha yenye lengo la kujadili mikakati ya kulitengeneza jengo hilo kati ya Wataalamu wa Unesco na Watendaji wa Serikali ya Zanzibar Waziri wa elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Lela Mohamed Mussa amesema hatua hiyo itaongeza fursa kwa Zanzibar kuimarisha sekta ya Utalii kutokana na kuutunza Mji Mkongwe na kuongeza hadhi ya Vivutio vyake. 

WEMA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA VYUO VIKUU VYA CHINA

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imesema ujio wa Wageni kutoka Chuo cha Hunan  Nchini China kutaendeleza Ushirikiano wa Kielimu  Zanzibar

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh Leila Muhammed Mussa amesema hayo Ofisini  kwake Mazizini wakati alipokuwa akizungumza na Wageni kutoka Chuo Kikuu cha Khunan Nchini China.

Amesema mambo mbali mbali wamekubaliana nao ikiwa ni pamoja kueka ushirikiano Mzuri katika mazingira ya Elimu kwa Wanafunzi wa Maandalizi, Secondari na Chuo Vikuu mbali mbali vilivyopo  Nchini

VETA NA KIST ZAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe Leila Mohamed Mussa amesema Serikali imekusudia kuzalisha Walimu wenye viwango kupitia ufundi na Mafunzo ya Amali. 

Waziri Lela ametoa Kauli hiyo, katika utiaji Saini kati ya Taasisi ya Sayansi na Ufundi (KARUME) na Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) kwa lengo la kukuza na kuzalisha Walimu wapya wenye uwezo wa kufundisha ufundi na Mafuzo ya Amali.

Mh: Lela amezipongeza Taasisi zote mbili na amesema hatua hiyo itasaidia kukuza umoja na ushirikiano kati ya Bara na Visiwani.

SMZ IMETENGA FEDHA KUJENGA UPYA DAHALIA YA SKULI YA UFUNDI KENGEJA

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa amewataka Wanafunzi wa Skuli ya Ufundi Kengeja kuitunza na kulinda vyema Miundo mbinu ya Skuli hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu.

Akikabidhi Eneo la Ujenzi wa Daghalia kwa Kampuni ya Ujenzi ya United Ramp kufuatia kuungua Moto kwa Bweni la Wanaume la Skuli hiyo Waziri lela amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu imetenga Fedha kwa ajili ya kujenga upya Daghalia hiyo hivyo amewataka Wanafinzi hao kuthamini Miundo mbinu hiyo kwa Maslahi yao na Vizazi vijavyo.

Subscribe to MHE. LELA MOHAMED MUSSA
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.