RAIS FILIPE NYUSI AFUNGUA MAONESHO YA 48 YA SABASABA

RAISI WA JAMUHURI YA TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi amefungua maonesho ya 48 ya Biashara ya kimataifa dar es salaam (sabasaba) 2024 huku akiwataka Washiriki wa maonesho hayo kuto jifungia ndani na badala yake kutafuta fursa za Masoko nje ya Nchi.

Akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa maonesho hayo akiwa Mgeni Rasmi Rais Nyusi ambaye yupo Nchini kwa ziara ya Siku Nne amewataka Wafanyabiashara wa Msumbiji na Tanzania kuendelea kushiriki ili kuweza kukuza Biashara zao.

Awali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia

Suluhu Hassan amewataka Wafanyabiashara wenye Bidhaa Zenye ubora kuzisajili katika Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) ili kuweza kupata Masoko Ndani na Nje ya Nchi.

Nae Waziri wa Biashara na maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omary Shaban amesema zaidi ya Kampuni 3846 kutoka Nchi 26

Duniani zinashiriki katika maonesho hayo kwa Mwaka 2024.

Kwa upande wake baadhi ya Taasisi zinazoshiriki katika Maonesho hayo zikiwemo Taasisi kutoka Zanzibar zimeeleza mafanikio ya Taasisi zao.

Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam (sabasaba) yanafanyika Jijini Dar Es Salaam ambapo Yameanza Juni 28 na yanatarajiwa kufungwa Julai 13 Mwaka Huu

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.