VIJANA WAMETAKIWA KUTUMIA VYEMA FURSA ZINAZOJITOKEZA NA KUPANGA MIKAKATI MADHUBUTI ITAYOSAIDIA KUPELEKA MBELE UMOJA NA MAENDELEO YA TAIFA.

MAKAMO WA PILI WA RAISI

Wito huo umetolewa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika Kongamano la kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 Mhe Hemed Suleiman Abdallah amesema hatua hiyo itasaidia kufikia malengo waliojiwekea ya kujikomboa Kielimu na kujiepusha na vishawishi kwa kuzingatia mila, silka na utamaduni wa Mzanzibar.

Hivyo ameitaka Wizara ya elimu na Mafunzo ya Amali kuendelea kushirikiana na Shirikisho La Vyuo Vikuu na Taasisi ya Elimu ya juu Zanzibar ZAHILFE ili kuweza kutatua matatizo wanayokutana nayo Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na kuhakikisha wanaendelea vizuri katika Masomoyao. 

Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdulgullam Hussein Gulam amesema Serikali imeona kuna umuhimu wa kuanzisha sheria mpya ya Bodi ya Mikopo ambayo italeta fursa kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na vyuo vya vyati kwa kupata mikopo pamoja na kuanzisha idara maalum  ya Vyuo Vikuu ambayo itashuhulikia matatizo ya Wanafunzi ikiwemo upatikanaji wa  mikopo na Bima ya afya.

Mwenyekiti wa ZAHILFE Makame Khamis Makame amewaomba Viongozi husika kuwa na ushirikiano mzuri baina ya na uwongozi ili kuweza kufikia malengo yao kwa ufanisi zaidi.            

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.