NAPOLI KUMKOSA ALEX MERET, MWEZI MMOJA KUTOKANA NA JERAHA

Alex Meret

Mabingwa watetezi wa Serie A Napoli watamkosa mlinda mlango wa kimataifa wa Italia Alex Meret kwa angalau mwezi mmoja baada ya kuumia misuli ya paja.

 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo, Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alipata jeraha hilo katika sare ya bila kufungana dhidi ya Monza Ijumaa iliyopita, huku uchunguzi ukionyesha kupasuka kwenye msuli wa paja la kushoto.

Ingawa klabu haikusema atakaa nje kwa muda gani, lakini kwa mujibu wa wataalamu, jeraha kama hilo kawaida huhitaji angalau wiki tano za kupona.

Napoli italazimika kumtegemea kipa chaguo la pili Pierluigi Gollini kwa mechi chache zijazo, ikiwa ni pamoja na mechi ya Kombe la Super Cup ya Italia dhidi ya Fiorentina Januari 18.

Napoli wanakabiliwa na kibarua kigumu kuhifadhi taji lao huku wakishika nafasi ya nane kwenye michuano ya Italia, alama 17 nyuma ya viongozi Inter Milan.

Watatumai Meret atarejea kwa wakati kwa mechi yao ya nyumbani ya 16 bora Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona mnamo Februari 21, na mkondo wa pili huko Uhispania mnamo Machi 12.

hot
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.