Wananchi wa jamii ya kimasai wanaoishi ndani ya hifadhi ya Ngorongoro wamefanya tamasha la kimila la kiutamaduni huku wakisema kwamba wataendelea kuhama kwa hiyari kuelekea katika Kijiji cha Msomera na maeneo mengine nchini Tanzania.
Kufanyika kwa tamasha hilo la kiutamaduni ambalo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa kabila hilo limefuta taarifa za uzushi za baadhi ya taasisi zinazojiita kuwa zinatetea haki za binadamu ambazo zimekuwa zikidai serikali ya Tanzania imekuwa ikiwahamisha kwa kuwalazimisha na kutumia nguvu kuinyanyasa jamii hiyo
Katika tamasha hilo la kiutamaduni jamii hiyo kuanzia katika rika la ujana wakiongozwa na wazee waliweza kufanya matambiko ya kimila ndani ya kreta bila kubughudhiwa na mtu yoyote na kuelezwa kwamba tukio hilo hufanyika kila baada ya miaka kumi.