Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar imefanikiwa kutekeleza zoezi la kujiandaa na kukabiliana na dharura za Ndege, hatua inayolenga kuimarisha uratibu kati ya Taasisi za Ulinzi, usalama na usimamizi wa maafa. Zoezi hilo limefanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Abeid Amani Karume
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Mulhat Yussuf Said wakati akizungumza na Waandishi wa Haaabari
Amesema hatua hiyo ni sehemu ya mikakati ya kuhakikisha usalama wa Abiria na miundombinu ya Viwanja vya Ndege, hususan wakati wa dharura za Ndege.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya kukabiliana na Maafa Zanzibar, Makame Khatib Makame amesema Zoezi hilo linaendana na sheria ya kukabiliana na maafa ya Mwaka 2015 pamoja na mpango wa Kitaifa wa dharura, akisisitiza kuwa hatua hiyo inaonesha utayari wa Taasisi za Serikali kujikinga na Majanga mbalimbali.
Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Abeid Amani Karume (AAKIA), Amani Hamdun Zubeir, Amesema lengo kuu la Zoezi hilo ni kupima ufanisi wa uratibu na ushirikiano kati ya Taasisi zote zinazohusika na usalama wa Viwanja vya Ndege.
Viwanja vya Ndege vimekuwa vikiongeza juhudi za kuimarisha usalama na utayari wa kukabiliana na dharura, kufuatia ongezeko la safari za Anga pamoja na mahitaji ya Viwango vya Kimataifa vya usalama wa Ndege.
