SERIKALI KUTUMIA BILIONI 79 KUJENGA VITUO VYA POLISI 698 NCHI NZIMA
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, amesema Serikali imepanga kutumia zaidi ya Shilingi Bilioni 79 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya polisi 698 nchini, ikiwa ni mkakati wa kuimarisha usalama wa raia na mali zao.
Akizungumza leo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya Vituo vya Jeshi la Polisi visiwani Zanzibar Mhe. Ayoub Mahmoud amebainisha kuwa uamuzi huo umekuja baada ya Serikali kuona kuna uhitaji wa kusogeza huduma za Kipolisi karibu na wananchi zaidi.




