KUWEPO KWA HAKI SAWA YA KIJINSIA KUMESAIDIA KUKUZA UCHUMI WA NCHI

WAZIRI RIZIKI PEMBE

    Kuwepo kwa haki sawa ya Kijinsia katika utendaji kazi kumechangia maendeleo imara ya kiuchumi.

    Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe.Riziki Pembe Juma amesema maadhimisho hayo ni ishara ya Maendeleo ya kiutendaji katika Serikali hali ambayo imechangia kukua kwa Sekta mbalimbali Serikalini kwa kuwepo kwa haki ya usawa wa jinsia katika nafasi mbalimbali za Uongozi.

    Akitoa salamu za Mkoa Katibu Tawala Mkoa wa Kusini Unguja Ndg.Radhia Rashid Haroub amesema Mkoa huo kwa kushirikiana na Vyomba vya Ulizi na usalama umeimarisha amani iliyopo Nchini ili shughuli za Kijamii ziende kwa haki na usalama .

    Mkurugenzi Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ndg.Siti Abasi Ali amesema Wizara hiyo inahakikisha inamlinda Mtoto dhidi ya vitendo vya udhalilishaji na kumuezesha Kielimu na kusaida Wajasiriamali Wanawake.

     Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa kila ifikapo Tarehe Nane ya Mwenzi Watatu ambapo kaulimbiu ya Mwaka huu ni Wekeza kwa Mwanamke Kwa Maendeleo Endelevu

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.