SMZ NA SMT ZAENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WAPIGANAJI NCHINI

Mafunzo kmkm

     Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimesema zinaendelea kuunga mkono juhudi za Wapiganaji kwa kuwajengea uwezo ili kufikia malengo ya Serikali.

     SMZ na SMT  akifunga Mafunzo ya Wanafunzi wa Uhamiaji wa kozi ya uendeshaji vyombo vidogo vidogo na uzamiaji, Naibu Meya wa Magharibi b,Ndg Khadija Omar Ngarama, amesema hatua hiyo itasaidia Wapiganaji kufanya kazi zao kwa urahisi.

   Mkuu wa Operation KMKM Captan, Ndg.Hussen Mohamed Seif, amesema Mafunzo hayo yatawawezesha kujiimarisha zaidi katika majukumu yao ya kila siku.

    Kamishna Msaidizi  Uhamiaji  Ndg.Muhsini Abdallah Muhsini, amesema wanashukuru kwa Mafunzo waliopatiwa kwa kuwa yatakwenda kudhibiti mipaka ya Nchi na kukiwezesha Kikosi chao kuondokana na changamoto iliyokuwa ikikabili.

    Akitoa taarifa ya mafunzo ya uhamiaji Mkuu wa Chuo KMKM LCDR Abdallah Hassan Mfamau amesema lengo la Chuo ni kutoa Askari waliobora na wenye nidhamu hivyo Chuo kinasimamia nidhamu ili kuwawezesha Askari hao kufanya kazi kwa ufanisi.

    Akisoma Risala ya Ufungaji wa mafunzo hayo Ndg. Constable Antony Emmanuel Chilala  amesema wamepata mafanikio mbalimbali ikiwemo kuwaandaa Maafisa na Askari wa Uhamiaji  katika uokozi uzamiaji uendeshaji wa vyombo vidogo vya Baharini.

   Akizungumzia matatizo katika kozi hiyo amesema ni pamoja na mahanga kwa wapiganaji  kukosekana na  huduma za Afya kambini huduma za kila siku kambini.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.